Baada ya kuwepo kwa maswali mengi kuhusu tabia ya mwanamziki na
muigizaji Hemedi Suleiman a.k.a PHD, kuwa anaringa sana, na ni mtu ambae
anapenda sana kuwa na watoto wa kike.
hiki ndicho alichokizungumza Hemedi leo hii kupitia xxl ya Clouds fm
"naomba jamani watu wajue kuwa mi siringi, ila watofautishe kati ya swag
na kuringa, unajua Hemedi Suleiman na PHD ni watu wawili tofauti,
nikiwa Hemedi sina mambo hayo kabisa, na nikiwa kama PHD hiyo is not me
ni kuigiza tu..ila the only reason guys wana hate ni kwasababu wana
deploma na nina PHD" amesema PHD.
Baada ya kumuuliza alipofikia kuhusu show yake aliyoiita "wife star
search" maalumu kwa ajili ya kufanya shows sehem mbali mbali kutafuta
mke hemedi alisema
"ile ilikua ni kwaajili ya kutafuta wife serious, ila baada ya kupokea
simu kadhaa kutoka kwa mashekhe na kuniuliza "baba ako alifanya
audition?" nikaona duuuh, wacha niachane nayo tu
Hemedi PHD kwa sasa ana ngoma yake inayofanya vizuri inayoitwa "going
crazy" aliyoifanya chini ya producer Pancho ndani ya B Hits