DJ NYASI24.COM

DJ NYASI24.COM

Friday, July 12, 2013

[Offical Music Video ]MALAIKA - Dogo scope & Tenya Brown

Kama kweli Bhakhresa atafanya hivi, wafuasi wake wataongezeka



996796_379903418798881_736826428_n
Hili ni dish la AzamTV ambayo inazungumziwa
 
Taarifa zilizoenea chinichini kwa sasa ni kwamba kuna kitu kingine kipya kutoka kwa kampuni ya Azam ambayo ni maarufu kwa kutengeneza bidhaa za vyakula, usafirishaji abiria kwa njia ya boti na hata michezo pia kupitia Azam FC ambapo kampuni hii inadaiwa kukaribia kutambulisha king’amuzi ambacho kitakua na uwezo wa kuonyesha Tv channel mbalimbali zikiwemo za Tanzania pia. Taarifa hizo za chinichini zimezidi kuamplfy kwamba gharama yake ya malipo ya kila mwezi itakuwa ndogo zaidi ya ving’amuzi vyote kwa Tanzania na watumiaji kwa kila mwezi watatakiwa k
Huu ni uwanja wanaoumiliki Azam FC Chamazi Mbagala Dar es salaam.
ulipia pesa za kitanzania Shilingi elfu mbili tu…… hata hivyo NYASI.COM. inazidi kufatilia kupata info zaidi

Unaambiwa hii ndio video mpya ya Mwanamke akimpiga mume wake hadharani Kenya

.
Ni ngumu kumuona mwanaume akitokwa machozi kama hivi…. hii imetokana na mke wake kumpiga makofi hadharani kwenye mji wa Meru nchini Kenya ambapo Mwanamke huyo alikua anadai jamaa kamkana, japo anasisitiza kwamba ni mume wake na ndio baba wa watoto mapacha akiwemo mmoja alienae mgongoni, Mwanaume alikataa kabisa na kusema hata watoto sio wake.
Taarifa ambayo imerushwa na KTN Kenya, ni kwamba alichotaka Mwanamke ni Mwanaume huyo akubali tu kwamba ni mume wake na pia ndio baba watoto wa mapacha hao… lakini Mwanaume aliapa kabisa kwamba hausiki kwenye upande wowote, hicho ndio kilichompa hasira Mwanamke na kuanza kumpiga na baadae pia kusaidiwa kupiga na Mwanamke aliekua nae.
Kenya imekua kwenye mfululizo wa kesi za Wanawake kupiga waume zao nyumbani na hadharani pale wanapokosana ambapo February 2012 Umoja wa Wanaume Kenya ulitangaza kususia kula majumbani kwa wiki moja na kununua chakula hotelini mpaka Serikali itakapoingilia usawa wa Wanaume na kuhakikisha tabia ya Wanawake kupiga Waume zao inamalizwa.

.

Thursday, July 11, 2013

hashim shedrack - pamsalaba.mp3 @Hulkshare:

 hashim shedrack - pamsalaba.mp3 @Hulkshare:

MAMA MZAZI WA PROFESA J AFARIKI DUNIA BAADA YA KUNGONGWA NA GARI USIKU WA LEO HUKO MBEZI JUU, DAR ES SALAAM

Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake.  Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'


HABARI ZILIZOPOKEWA USIKU HUU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU BAADA YA KUGONGWA NA GARI  MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.

PROFESA J AMETHIBITISHA  HILO MUDA MFUPI ULIOPITA, NA KUSEMA INAMUIA VIGUMU KUAMINI IMETOKEA KWANI ANASEMA MAREHEMU MNAMO SAA MBILI HIVI ALIMPIGIA SIMU NA KUMWELEZA KUWA AMEPATA AJALI NA KWAMBA WAKATI HUO YUKO KITUO CHA POLISI, BILA SHAKA KUPATA FOMU YA PF 3 YA KUMUWEZESHA KWENDA KUTIBIWA HOSPITALI.

"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NA GARI....NJOO NIKO POLISI NAANDIKISHA....MWANANGU NAKUFA....ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU.

ANASEMA WAKATI ANAPIGIWA SIMU NA MAMA YAKE YEYE ALIKUWA KATIKA MGAHAWA WA NYUMBANI LOUNGE, NAMANGA, DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA KATIKA KIKAO NA LADY JAY DEE NA MUMEWE GADNA G. HABASH, AMBAO BAADA YA TAARIFA HIYO WALIMSINDIKIZA HADI HOSPITALI YA TUMBI.

"TULIPOFIKA HOSPITALI SIKUAMINI KUONA BADALA YA KUPELEKWA WODINI AMBAKO NILIDHANI MAMA ATAKUWA AMELAZWA NIKAPELEKWA CHUMBA CHA MAITI AMBAKO NILIMKUTA MAMA AKIWA MAREHEMU", ALISEMA PROFESA J KWA MAJONZI.

GLOBU YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA PROFESA J KWA MSIBA HUU MZITO NA WA KUSIKITISHA. TUNAMWOMBA MOLA AMPE NGUVU YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. 

TUTAENDELEA KUWAPASHA KINACHOJIRI KADRI HABARI  ZAIDI ZITAPOPATIKANA. KWA SASA PROFESA J NA WADAU WENGINE WAKO NYUMBANI KWAKE MBEZI JUU.

Tuesday, July 2, 2013

MMILIKI WA FACEBOOK AKISHEREKEA KUPITISHWA KWA NDOA YA JINSIA MOJA

Mmiliki wa mtandao wa kijamii Facebook CEO Mark Zuckerberg amejiunga na wafanyakazi wa kampuni yake waliozidi 700 katika matembezi ya kusherekea maamuzi ya mahakama kuhusu haki za ndoa ya jinsia moja. Matembezi haya yamefanyika mitaa ya San Francisco Jumapili Asubuh. Kwa mujibu wa Wall Street Journal asilimia 15 ya wafanyakazi wa facebook.

Sheria hio inayo sherekewa Imeruhusu wanandoa wa jinsia moja kumiliki leseni ya ndoa ndani ya siku 30 baada ya kuoana. 

DENIS LUKOSI - MUNGU KAFANYA YAKE